SHERMAN WA YANGA AIFUNGIA LIBERIA IKICHAPWA 2-1 NA NIGERIA MECHI YA KUSTAAFISHA JEZI YA WEAH MONROVIA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SHERMAN WA YANGA AIFUNGIA LIBERIA IKICHAPWA 2-1 NA NIGERIA MECHI YA KUSTAAFISHA JEZI YA WEAH MONROVIA

Na Mwandishi Wetu, MONROVIA
MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga, Kpah Sherman jana aliifungia timu yake ya taifa, Liberia ikichapwa 2-1 na Nigeria katika mechi ya kuistaafisha jezi ya gwiji na Rais wa nchi hiyo, George Weah.
Rais wa Liberia, George Weah jana aliichezea mechi ya kirafiki nchi yake akiwa ana umri wa miaka 51 ikifungwa 2-1 na Nigeria mjini Monrovia.
Weah, mwanasoka wa kwanza wa Afrika kushinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Dunia wa FIFA, alicheza kwa dakika 79 iliyoandaliwa maalum kuistaafisha jezi namba  14 iliyokuwa inatumiwa na gwiji huyo enzi zake.
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Kpah Sherman akiifungia Liberia kwa penalti jana

Rais wa Liberia, George Weah jana aliichezea Liberia akiwa ana umri wa miaka 51 

Mshambuliaji huyo wa zamani wa AC Milan, aliyechaguliwa kuwa Rais wa Liberia Januari mwaka huu, alipewa heshia maalum wakati anatolewa uwanjani.
Nigeria iliteremsha kikosi chake kamili kilichohusisha nyota wake kama Wilfred Ndidi wa Leicester City na kiungo mwenzake, ... Continue reading ->
Source: Bin ZuberyRead More