SHIBUDA AWAGEUZIA KIBAO VYAMA VYA SIASA KUHUSU LUGHA WANAZOTUMIA KUMSHAURI RAIS - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SHIBUDA AWAGEUZIA KIBAO VYAMA VYA SIASA KUHUSU LUGHA WANAZOTUMIA KUMSHAURI RAIS

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii 
*Awaambia zama zimebadilika …hii ni Awamu ya Tano

MWENYEKITI wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini John Shibuda amewashauri viongozi wa vyama vya siasa kuwa makini na matumizi ya lugha wanayotumia pindi wanapotaka kumshauri Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano Dk.John Magufuli.

Wakati huo huo amewahakikishia kuwa Rais Magufuli hawezi kuufuta mfumo wa vyama vingi bali kilichopo anaviimarisha na kwamba ipo siku atazungumzia hilo kwa kina.Shibuda ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati viongozi wa vyama vya siasa nchini vilipokutana kwa lengo la kujadili mabadiliko ya kikatiba na kisheria kuhusu uchaguzi kabla ya Uchaguzi kuu wa mwaka 2020.

Katika mkutano huo ambao umeandaliwa na Jukwa la Katiba Tanzania (Jukata),Shibuda amesema ni vema wanasiasa wakawa makini katika matumizi ya lugha hasa kwa kuzingatia zama zimebadilika.Amesema lugha ambazo walikuwa wanazitumia katika awamu zilizopita lazima wanasiasa wajue zama hizi hazina nafasi na hivyo ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More