Shilingi Bilion tano zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Studio za redio na luninga za TBC Jijini Dodoma - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Shilingi Bilion tano zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Studio za redio na luninga za TBC Jijini Dodoma

Na Shamimu Nyaki –WHUSMSerikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni tano kwa ajili  ya ujenzi wa studio za Redio na Runinga  za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)  katika makao makuu ya nchi Dodoma.Hayo yamesemwa leo Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Sera,Bunge,  Kazi ,Ajira, Vijana na wenye ulemavu Mhe. Antony Mavunde alipokua akijibu swali la Mhe. Anna Richard Lupembe (Viti Maalum) kwa niaba ya Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe aliyeuliza ni lini Redio Tanzania (TBC Taifa) itasikika katika kata za Ilela na Ilunde Wilayani Mlele.Akijibu swali hilo Mhe. Mavunde amesema kuwa Serikali inaendelea na jitihada za kupanua usikivu wa TBC katika  Mikoa na Wilaya ambazo  hazina usikivu au kuwa na usikivu hafifu  ambapo katika bajeti ya mwaka 2016/2017 kiasi cha shilingi Bilioni moja zilitengwa kwa ajili ya kupanua usikivu katika wilaya tano za mpakani mwa nchi.“Mkakati wa Serikali ni  kujenga mitambo ya redio katika mikoa ya Songwe,Katavi,Njo... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More