SHIRIKA LA GREAT HOPE WATOA TUZO KWA WASHIRIKI WA UWEZO AWARD - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SHIRIKA LA GREAT HOPE WATOA TUZO KWA WASHIRIKI WA UWEZO AWARD

 SHIRIKA la Great Hope Foundation leo limetoa tuzo kwa washiriki wa mradi wa UWEZO AWARD katika sherehe zilizofanyika chuo kikuu cha Dar es Salaam leo katika shule za Sekondari za hapa nchini.
 Mradi huu unaendeshwa kwa njia ya mashindano ambapo wanafunzi hushindana kutumia uwezo wao kufanya kazi mbalimbali za kijamii ambazo wao wanachagua kufanya.
UWEZO AWARD ina malengo makuu matano ambayo ni  Kuwatengenezea wanafunzi jukwaa la kujitambua/kufahamu uwezo/vipaji walivyonavyo ( hata vile ambavyo havionekani zaidi darasani.
Kuwapa wanafunzi jukwaa la  kujifunza uongozi  Kuwapa wanafunzi jukwaa la kujifunza kuwajibika na kuwa mstari wa mbele kutatua changamoto zinazoikabili jamii inayowazunguka, Kutambua na kutoa tuzo kwa miradi bunifu iliyofanywa na wanafunzi katika UWEZO AWARD na  Kukuza na kuwajengea wanafunzi ujuzi katika maeneo ambayo wanafunzi wameonesha UWEZO.Washindi wa kwanza wa tuzo za UWEZO AWARD wakipokea tuzo yao kutoka kwa mgeni rasmi Maida waziri mara baada ya kuibuka kide... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More