Shirika la Sun Flower kujenga kiwanda nchini - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Shirika la Sun Flower kujenga kiwanda nchini

Shirika la Kimataifa linalojishughulisha na uzalishaji wa Kilimo cha Alizeti {Sun Flower } la Alemdar kutoka Nchini Uturuki limeonyesha nia ya kutaka kujenga kiwanda kitakachozalisha Bidhaa tofauti kwa kutumia malighafi ya Maua hayo katika azma ya kuitikia wito wa Serikali wa kuwa Nchi ya Viwanda katika kipindi kifupi kijacho.
Ofisa Mkuu wa Shirika hilo Bibi Fatma Atala alieleza hayo wakati Ujumbe wa Viongozi wa Shirika hilo ulioongozwa na Mwenyekiti wake Bwana Oktay Alemder ulipokutana kwa mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Vuga Mjini Zanzibar.
Bibi Fatma Atala alisema Mradi huo wa Kibiashara endapo utafanikiwa kuanzishwa Visiwani Zanzibar unalenga pia kuwashirikisha moja kwa moja Wakulima Vijini kwa kulima Maua ya Alizeti katika baadhi ya maeneo yao ya Kilimo.
Alisema Maua ya Alizeti ni bidhaa inayoendelea kuwa na hadhi kubwa katika masoko ya Kimataifa ambayo inaweza kusaidia kunyanyua mapato ya washiriki katika ukulima wake sambamba na kuongeza Map... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More