SHIRIKA LA WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA WA KIMAREKANI LA PEACE CORPS LAWAAPISHA WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA 59 WA SEKTA YA ELIMU - Kajunason | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SHIRIKA LA WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA WA KIMAREKANI LA PEACE CORPS LAWAAPISHA WAFANYAKAZI WA KUJITOLEA 59 WA SEKTA YA ELIMU

Kaimu Balozi wa Marekani nchini Dk. Inmi Patterson aliongoza hafla ya kuapishwa kwa wafanyakazi wa kujitolea wa Kimarekani wa Peace Corps wapatao 59 watakaohudumu nchini Tanzania kwa miaka miwili katika sekta ya Elimu. Wafanyakazi hawa watapangiwa kufanyakazi katika wilaya 35 nchini kote Tanzania.
Dk. Patterson aliongoza kiapo rasmi cha wafanyakazi hao wapya wa kujitolea mbele ya mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe.William Tate Olenasha. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na viongozi wa serikali, wafanyakazi wa kujitolea wa zamani wa Peace Corps, wawakilishi wa taasisi wabia na wanafamilia wa familia za Kitanzania ambazo wafanyakazi hawa wa kujitolewa waliishi nazo. 
Kaimu Balozi Patterson aliwaeleza wafanyakazi wapya wa kujitolea kuwa: "Wakati ambapo ninyi mnaweza kuwa Wamarekani wa kwanza kukutana na kufanya kazi na wafanyakazi wenzenu na majirani zenu wa Kitanzania, ni dhahiri kwamba katika mawazo yao mtaendelea kuwa wawakilishi wa watu wa Marekani na ubia wa muda m... Continue reading ->


Source: KajunasonRead More