SHIRIKISHO LA SOKA DUNIANI LAKATAA KUONGEZA IDADI YA TIMU KOMBE LA DUNIA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SHIRIKISHO LA SOKA DUNIANI LAKATAA KUONGEZA IDADI YA TIMU KOMBE LA DUNIA

SHIRIKISHO la Soka Duniani (FIFA) limekataa kuongeza idadi ya timu zitakazoshiriki kwenye michuano ya Kombe la Dunia ya 2022 itakayofanyika Qatar, kutoka timu 32 hadi 48 kama ambavyo ilikuwa imependekezwa.
Kwa mujibu wa FIFA imesema kuwa baada ya majadiliano ya kina na wadau wote muhimu sasa  imeamua kwamba chini ya mazingira ya sasa haitaweza kulitekeleza pendekezo hilo kwa wakati huu.
Hivyo michuano hiyo sasa itasalia na timu 32 za awali na hakutakuwa na pendekezo litakalowasilishwa kwenye kongamano lijalo la FIFA litakalofanyika Juni 5.
Uamuzi huo wa mwisho wa FIFA umetolewa mapema tofauti na ilivyotarajiwa kwamba yangetolewa wakati wa kongamano hilo litakalofanyika Paris nchini  Ufaransa kabla ya michuano ya Kombe la Dunia ya wanawake.
Rais wa FIFA, Gianni Infantino aliunga mkono pendekezo hilo, na maamuzi haya yanatajwa kuwa pigo kubwa kwake.... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More