SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WACHIMBA MADINI NCHINI YASIKILIZA KERO ZA WACHIMBAJI WA MKOA DAR,PWANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WACHIMBA MADINI NCHINI YASIKILIZA KERO ZA WACHIMBAJI WA MKOA DAR,PWANI

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

SHIRIKISHO la Vyama vya Wachimbaji wa Madini nchini (FEMATA) limefanya ziara ya kutembelea wachimbaji wa Mkoa Dar es salaam na Pwani ambapo wametumia nafasi hiyo kutoa elimu kwa wachimbaji pamoja na kusikiliza kero na kutatua.

Ziara hiyo iliongozwa na Rais wa FEMATA John Bina akiwa ameambatana na uongozi wa chama cha wachimbaji Mkoa wa Dar es salaam na Pwani (DARCOREMA) ambapo pia ujumbe huo ulitembelea wadau wa sekta ya madini wakiwemo wazalishaji na wasambazaji wa vifaa vya wachimbaji vikiwemo Baruti na mitambo ya inayotumiwa na wachimbaji.

Kwa mujibu wa Bina wachimbaji kupitia vyama vyao hawana budi kutatua changamoto zao kupitia meza ya mazungumzo baina hao na Serikali.

Mojawapo ya kero zilizoonekana kukithiri Kwa wachimbaji ni pamoja na wengi wao kukosa mitaji na hivyo kulazimika kuingia ubia na wawekezaji wa Nje makubaliano ambayo Mara nyingi ukosa usawa kibiashara.

Pia Bina amesema tayari shirikisho limeandaa mpango wa namna ya kuwasaidia... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More