SHUBASH PATEL ATOA MABATI 1,000 KUIMARISHA SEKTA YA ELIMU PWANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SHUBASH PATEL ATOA MABATI 1,000 KUIMARISHA SEKTA YA ELIMU PWANI


NA MWAMVUA MWINYI,PWANI 

SEKTA ya elimu mkoani Pwani, inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa 3,678 katika shule za msingi pamoja na nyumba za walimu 5,188.


Kufuatia changamoto hiyo ,kampuni ya Sayona fruits ,iliyopo Mboga huko Chalinze imetoa mabati 1,000 yenye thamani ya sh.mil 24 ,kwa ajili ya umaliziaji wa majengo mbalimbali ya shule za msingi mkoani humo .

Akipokea mabati hayo ,kutoka kwa mkuu wa kitengo cha mahusiano cha kampuni hiyo ,Abubakar Mlawa , mkuu wa mkoa wa mkoa huo mhandisi Evarist Ndikilo alisema ,wanakabiliana na changamoto hizo kwa kushirikiana na halmashauri,jamii na wadau wa elimu . “Miundombinu ya shule za sekondari na hasa shule za msingi bado kuna upungufu ,ambapo mkoa una jumla ya shule za msingi 613 huku za serikali zikiwa ni 562 na 51 ni za watu binafsi “

“Shule za msingi pekee mahitaji ya vyumba vya madarasa ni 700,671, yaliyopo 3,993 na upungufu ni vyumba vya madarasa 3,678 ” alifafanua Ndikilo. Ndikilo alitaja p... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More