SHULE BORA YA WATOTO WALIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI KUJENGWA WILAYANI SAME. - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SHULE BORA YA WATOTO WALIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI KUJENGWA WILAYANI SAME.

Shirika la New Dawn Communities linalofanya kazi kata ya Njoro iliyoko Wilayani Same kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo toka Califonia nchini Marekani wameamua kujenga Shule hio tarajiwa  ambayo inategemea kupokea watoto yatima na walemavu kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita. Jiwe la msingi upande wa mabweni limewekwa na DC wa Same Mh. Rosemary Senyamule na Mch. Ron kutoka Marekani ambapo linategemea kupokea wanafunzi kuanzia Januari, 2019. Wadau wamepania kujenga pia tawi la Chuo kikuu cha Pippeliner (kilichopo Marekani)  katika eneo hilo. Waanza kushirikisha waliosoma chuo hicho kuchangia. 
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Sitaki amewakumbusha kufuata sheria na taratibu za nchi zinazohusiana na mradi huo. Pia kawaasa kuweka utaratibu mzuri wa kuwapata watoto hao; na ametoa wito kwa wazazi na wananchi kutumia fursa hiyo badala ya kuwafungia watoto walemavu nyumbani. Mchungaji Mshomi ambaye ndiye mkurugenzi wa taasisi hiyo, amesema wanategemea kupokea wanafunzi zaidi ya 600 wenye uhitaji na kuwasomesha. Pia wanaendelea kushirikiana na jamii kwa huduma nyingine kama kilimo cha bustani, huduma ya maji bure, ujenzi wa barabara na wamekusudia kujenga uwanja wa kisasa wa mpira. Ameiomba jamii kuwapa ushirikiano. " Nawashukuru kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kutoa elimu bure na sera ya nchi inayotoa haki sawa ya elimu kwa watoto wakiwemo yatima na walemavu, asanteni sana"lisema DC Same. 
Yafuatayo yanafurahisha: Njoro uwanja wa mpira wa kisasa!Njoro chuo kikuu.Hakika" Same is not same"

Uwekaji wa jiwe la msingi upande wa mabweni limewekwa na DC wa Same Mh. Rosemary Senyamule na Mch. Ron kutoka Marekani ambapo linategemea kupokea wanafunzi kuanzia Januari, 2019.  Sherehe za uwekaji jiwe la msingi Picha ya pamojaSame is not the same!


Source: Issa MichuziRead More