Shule ya Msingi ya Uzuri yapata Maktaba - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Shule ya Msingi ya Uzuri yapata Maktaba

Na Mwandishi wetu,Wanafunzi nchini wametakiwa kujibidisha kusoma vitabu mbalimbali sio kwa malengo ya kufaulu mitihani pekee, bali  pia kwa ajili kupata elimu na maarifa mapya yatakayowasaidia kukabiliana na changamoto za maisha.Mkurugenzi wa Taasisi ya Dr. Ntuyabaliwe Jacqueline Mengi ametoa wito huo jijini Dar es salaam wakati akizindua maktaba ya shule ya Msingi Uzuri, iliyopo Kata ya Manzese, Manispaa ya Ubungo, ambayo imekarabatiwa na kuwekwa vitabu kwa hisani ya taasisi hiyo.Mkurugenzi huyo pia amewashawishi wanafunzi wa shule za msingi nchini wa kuanzia darasa la nne hadi la saba kushiriki shindano la Andika Challenge la kuandika na kubuni hadith zenye mafundisho, lililoanzishwa na Taasisi hiyo,  na kuwahakikishia kuwa kila mkoa utatoa washindi.Wakizungumza katika hafla hiyo Afisa Elimu wa Manispaa ya Ubungo Chausiku Masegenya, na Mwenyekiti wa Kamati ya shule Bw. Yassin Shaaban Bakari wameipongeza Taasisi ya Dr Ntuyabaliwe kwa ufadhili huo unaounga mkono jitihada za serikali ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More