SHULE YA SEKONDARI MAKONGO YAMUENZI BABA WA TAIFA, MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE KWAKUTOA MISAADA HOSPITALI YA MWANANYAMALA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SHULE YA SEKONDARI MAKONGO YAMUENZI BABA WA TAIFA, MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE KWAKUTOA MISAADA HOSPITALI YA MWANANYAMALA

Na Karama Kenyunko, Blogu ya Jamii  Katika kumuenzi baba wa Taifa mwalimu Julius Nyerere, Shule ya Sekondari ya Makongo imefanya  shughuli mbalimbali  katika Hospital ya Mwananyamala ikiwa ni pamoja na kufanya usafi Kuchangia Damu na kutoa kutoa msaada wa Maji .
Shughuli hiyo  imeanza kwa maandamano na imeongozwa na mbunge wa Kinondoni Abdallah Mtulia kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Daniel Chongolo.
 Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya kumaliza kutembelea Hospitali hiyo na kukabidhi misaada mbali mbali Mkuu wa Shule ya Makongo, KanaliBYuda Kitinya amesema kuwa lengo kubwa la kufanya zoezi hilo ni kuwafundisha wanafunzi wa shule hiyo uzalendo  kama baba wa Taifa alivyokuwa akifundisha ambae alikuwa  anasisitiza uzalendo  katika nchi.
"Tunawafundisha vijana wetu uzalendo ili wafahamu kwamba ukiwa kijana unajukumu la kujitoa kwa ajili ya jamii inayokuzunguka kwani ninaimani kama tukiwafundisha na wakaelewa basi wataendelea kuelimisha wenzao na kujitoa siku hadi siku katika ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More