SIFURAHISHWI NA KASI YA MKANDARASI ALIEYEPEWA TENDA YA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI WILAYANI KIBONDO,KAKONKO MKOANI KIGOMA-NAIBU WAZIRI MGALU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIFURAHISHWI NA KASI YA MKANDARASI ALIEYEPEWA TENDA YA KUSAMBAZA UMEME VIJIJINI WILAYANI KIBONDO,KAKONKO MKOANI KIGOMA-NAIBU WAZIRI MGALU

Moureen Rogath, Kibondo. 
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu, amesema hajafurahishwa na kasi ya mkandarasi wa kampuni ya Urban and Engineering Service aliyepewa tenda ya kusambaza umeme vijijini katika wilaya ya Kibondo na Kakonko mkoani Kigoma. 
Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nyange, kata ya Mabamba na kusema kuwa endapo mkandarasi huyo hatobadilika katika utendaji wake serikali itamchukulia hatua za kisheria.
Naibu Waziri alisema wilaya ya Kibondo ni vijiji 3 vilivyowashwa umeme kati ya 40 huku wilaya ya Kakonko vijiji 5 vimewashawa kati ya 29 na kwamba hadi June 2020 vijiji vyote vinatakiwa kuwaka umeme. 
"Dhamira ya serikali ni kuona watanzania wote wanapata umeme kwenye makazi yao na kuwataka wananchi katika maeneo ya vijijini kuchangamkia fursa hiyo," amesema Naibu waziri huyo. 
Mapema akizungumza mkuu wa wilaya ya Kibondo Louis Bura, ameishukuru serikali kwa kuipa kipaumbele wilaya hiyo kupata nishati umeme kwa mara ya kwanza katika kijiji hicho.
Hata hivyo mkanadar... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More