siku 3 kuelekea Urusi, majeruhi yazidi kukiandama kikosi cha Argentina - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

siku 3 kuelekea Urusi, majeruhi yazidi kukiandama kikosi cha Argentina

Na Elizabeth lyavule.


vijana wa kocha Jorge Sampaoli wameshawasili nchini Urusi tayari kwa michuano ya kombe la dunia huku karata yao ya kwanza wakitegemea kuitupa kukabiliana na timu ya taifa ya Iceland siku ya ijumaa tarehe 16 saa 10 jioni kwa masaa ya Afrika Mashariki.Wakijawa na matumaini mengi yakubeba kombe la dunia nchini urusi baada ya kupoteza mchezo wa fainali zilizopita dhidi ya Ujerumani kule Brazil, kikosi chao kikiongozwa na Leonel Messi kimezidi kuandamwa na rundo la majeruhi kwa baadhi ya nyota wao muhimu.Alianza golikipa wao namba moja Sergio Romero aliepata maumivu ya bega katika siku za mwanzo za maandalizi ya fainali hizi za 21 pale Urusi, haikuishia hapo walimpoteza kiungo wao muhimu Manuel Lanzini aliyepata maumivu ya goti siku ya ijumaa hivyo kufanya wote wawili kuzikosa fainali hizo.Sasa ni zamu ya kiungo mkongwe Eva Bannega ameshindwa kuungana na wenzie kufanya mazoezi kwa siku mbili kutokana na kuwa majeruhi hivyo wanamuangalizia kama ataweza endelea na ... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More