SIKU YA AFRIKA YAADHIMISHWA KWA VIJANA KUPATA SOMO KUTOKA KWA WAZEE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIKU YA AFRIKA YAADHIMISHWA KWA VIJANA KUPATA SOMO KUTOKA KWA WAZEE

* Rais Magufuli atawala mdahalo apewa sifa katika kuongoza mapambano ya kiuchumi
Na Leandra Gabriel, Blogu ya jamii
MAADHIMISHO ya siku ya Afrika yanayoadhimishwa kila tarehe 25 mwezi Mei, kwa mwaka huu yameadhimishwa kwa jukwaa la tafakuri lenye kauli mbiu ya "Uafrika wetu na rasilimali za Bara letu ni urithi wetu" huku vijana wakipata somo kutoka kwa wazee na wapigania uhuru wa taifa.
Akizungumza katika tafakuri  hiyo ya pili Waziri wa Habari, sanaa, vijana utamaduni na michezo Dkt. Harison Mwakyembe amesema kuwa viongozi wa Afrika watakumbukwa kwa mengi waliyoyafanya pamoja na juhudi na jitihada walizozifanya zitaishi daima na kumbukumbu zao zitahifadhiwa daima na hadi sasa  zaidi ya kumbukumbu 256 zimehifadhiwa na amewataka vijana kujifunza kutoka kwa watetezi hao.
Mwakyembe amesema kuwa wao kama wizara wataendelea kuhifadhi mazuri yote yaliyofanywa pamoja na kuyaendeleza na hiyo ni pamoja na kuifanya lugha ya Kiswahili kuwa Lugha inayounganisha bara la Afrika.
Aidha amesema kuwa vijana... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More