SIMANJIRO WAZINDUA UGAWAJI VITAMBULISHO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMANJIRO WAZINDUA UGAWAJI VITAMBULISHO

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Tumaini Magessa amezindua utoaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara wadogowadogo kwa kuwataka wafanyabiashara wakubwa na wakati kutojihusisha na zoezi hilo.  Magessa aliyasema hayo mji mdogo wa Mirerani, wakati wa kugawa vitambulisho kwa wafanyabiashara wadogo.
Magessa alisema wafanyabiashara waliosajiliwa kwenye mfumo wa mamlaka ya mapato nchini (TRA) hawapaswi kupatiwa vitambulisho hivyo. "Serikali ipo pamoja nanyi wafanyabiashara wadogo, ndiyo sababu Rais John Magufuli akawatambua na kuagiza vitambulisho vyenu vitengenezwe," alisema Magessa. 
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Yefred Myenzi alisema wafanyabiashara wanapaswa kuwa wazalendo kwa kulipa kodi ili kufanikisha maendeleo. "Kupitia kodi ndiyo serikali inafanikisha maendeleo mbalimbali ikiwemo kujenga vyumba vya madarasa yahoo shule za sekondari na msingi ambavyo watoto wetu watasoma," alisema  Myenzi.  Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sima... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More