SIMBA B YAANZA VYEMA KOMBE LA UHAI, PRISONS, NDANDA, STAND NAZO ZASHINDA UDOM - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMBA B YAANZA VYEMA KOMBE LA UHAI, PRISONS, NDANDA, STAND NAZO ZASHINDA UDOM

Na Mwandishi Wetu, DODOMA
MABINGWA watetezi, Simba SC wameanza vyema michuano ya Ligi Kuu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20, inayoshirikisha vikosi vya pili vya klabu za Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo viwanja vya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwa ushidi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida United.
Ushindi huo katika mchezo huo wa Kundi B umetokana na mabao ya Meshack Abel dakika ya 19 na Modest Matinyange dakika ya 78, wakati bao pekee la Singida limefungwa na Said Habib dakika ya 90.
Mechi nyingine ya Kundi B leo, Stand United imeichapa Njombe Mji FC 1-0, bao pekee la Frank Zakaria dakika ya 88.

Mechi nyingine mbili za Kundi D leo, Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Lipuli FC mabao ya Abubakar Maulika dakika ya 43 na Ramadhan Ibata dakika ya 66, wakati Ndanda FC imeilaza 2-1 Kagera Sugar, mabao ya washindi yakifungwa na Juma Said Athumani dakika ya 42 na Yassin Hamad Rashid dakika ya 60 dhdii ya la Haroun Ally Said dakika ya 88.
Michuano hiyo itaendelea kesho…... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More