Simba Day imetisha nje na ndani - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Simba Day imetisha nje na ndani

August 8, 2018 Simba imeendelea na utamaduni wake wa kutambulisha wachezaji kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa mashindano mbalimbali ikiwa ni pamoja na ligi kuu Tanzania bara.


Simba imefanikiwa kuujaza uwanja wa taifa, kwa mujibu wa takwimu za Azam TV, zaidi ya mashabiki 53,000 walikuwepo uwanjani kushuhudia sherehe ya Simba Day.


Tamasha hili linazidi kuwa kubwa kadiri miaka inavyozidi kwenda mbele, msimu huu Simba wamefanikiwa nje na ndani ya uwanja.


Ukubwa au jinsi brand yao kama taasisi inavyozidi kukua. Hakuna shaka kabisa kwa kadiri siku zinavyozidi kwenda Simba wamehakikisha wanaiweka juu timu yao.


Wamei-market brand yao ndio maana wamejaza uwanja wa taifa wakiwa wao peke yao. Ni tukio ambalo lilikuwa linaoneshwa LIVE Azam TV lakini uwanja ulijaa.


Yanazungumzwa mengi kwamba, kwakua mechi zinaoneshwa kwenye TV ndio maana viwanja havijai na vilabu vinakosa Gate Collections lakini Simba wameiua hiyo dhana, mechi inaweza ikaoneshwa kwenye TV lakini watu wakaenda uwanjani kwa ajili ya ... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More