SIMBA QUEENS YACHEZA MECHI MBILI MFULULIZO SIKU MOJA, YASHINDA NA KUTOA SARE - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMBA QUEENS YACHEZA MECHI MBILI MFULULIZO SIKU MOJA, YASHINDA NA KUTOA SARE

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya Simba Queens jana imecheza mechi mbili za kujipima nguvu katika ziara yake ya nchini Ujerumani na kushinda moja na kutoa sare moja.
Kwa mujibu wa Mratibu wa Simba Queens, Suleiman Makanya mechi za jana zilikuwa ni dhidi ya timu za St Pauli.
Makanya mechi alisema ya kwanza walicheza na timu B ya St Pauli B na kushinda 3-1 wakati ya pili walicheza na timu A ya St Pauli na kutoka sare ya 2-2.

Nahodha wa Simba Queens akipokea msaada wa jezi baada ya mechi na St Pauli

Wachezaji wa Simba Queens katika picha ya pamoja na St Pauli

Mabao yote ya Simba Queens yalifungwa Amina Ramadhani mawili kwenye mechi ya kwanza moja mechi ya pili na Mwanahamisi Omar ‘Gaucho’ moja katika kila mechi.... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More