SIMBA SC HOI KENYA…YATOBOLEWA ‘TUNDU MBILI’ NA GOR MAHIA NA KUIKOSA SAFARI YA UINGEREZA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMBA SC HOI KENYA…YATOBOLEWA ‘TUNDU MBILI’ NA GOR MAHIA NA KUIKOSA SAFARI YA UINGEREZA

Na Mwandishi Wetu, NAKURU
KWA mara ya pili mfululizo, Gor Mahia ya Kenya imebeba taji la SportPesa Super Cup baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba SC ya Dar es Salaam, Tanzania.
Mashujaa wa Gor Mahia leo wameendelekuwa wanasoka wa kimataifa wa Rwanda, Meddie Kagere na Jaqcues Tuyisenge waliofunga mabao hayo, moja kila kipindi na kurudia mafanikio ya mwaka jana mjini Dar es Salaam wakiwafunga mahasimu wao wa Kenya, AFC Leopard 2-1 na kutwaa taji hilo. 
Kagere alianza kufunga bao zuri dakika ya sita akimalizia kazi nzuri ya George Odhiambo ‘Blackberry’ kabla ya Tuyisenge kufunga la pili akimalizia krosi ya Humphrey Mieno dakika ya 54.

Wanasoka wa kimataifa wa Rwanda, Meddie Kagere (kushoto) na Jaqcues Tuyisenge (kulia) wakishangilia baada ya kufunga leo 

Simba SC ilicheza ovyo kipindi cha kwanza na kuzidiwa kabisa na Gor Mahia, lakini kipindi cha pili ilibadilika na kutulia kujaribu kucheza soka ya maelewano, ingawa tayari wapinzani wao walikuwa wamekwishajipanga kuulinda ushindi... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More