SIMBA SC KUONDOKA KESHO MAPEMA TU KUIFUATA NDANDA MTWARA, MECHI JUMAMOSI NANGWANDA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMBA SC KUONDOKA KESHO MAPEMA TU KUIFUATA NDANDA MTWARA, MECHI JUMAMOSI NANGWANDA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KIKOSI cha mabingwa wa Tanzania Bara, Simba kinatarajiwa kuondoka kesho kwenda Mtwara kwa ajili ya mchezo wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Ndanda FC.
Wachezaji wote wanne kati ya watano walioruhusuiwa kwenda kuchezea timu zao za taifa kwenye mechi za Kimataifa wikiendi iliyopita wamerejea kasoro mmoja tu, kiungo Mzambia Cletus Chama ambaye anatarajiwa kuwasili kesho mapema na kuungana na wenzake kwa safari ya Mtwara.
Lakini Waganda beki Juuko Murshid, mshambuliaji Emmanuel Okwi na Wanyarwanda kiungo Haruna Niyonzima na mshambuliaji Meddie Kagere wamerejea na jana jioni wamefanya mazoezi.
Kocha Mbelgiji Patrick J Aussems atachukua wachezaji 20 kati ya wote kwa safari ya Mtwara, ambako timu inakwenda kucheza mechi ya kwanza ya ugenini na ya tatu kwa ujumla ya msimu baada ya kushinda mbili za awali nyumbani dhidi ya timu za Mbeya, Tanzania Prisons 1-0 na City 2-0.

Lakini kiungo Muzamil Yassin aliyeoa wiki iliyopita hatarajiwi kuwa miongoni mwa w... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More