SIMBA SC YAANZA VYEMA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA, YAWAPIGA WAARABU 3-0 - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMBA SC YAANZA VYEMA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA, YAWAPIGA WAARABU 3-0

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SIMBA SC imeanza vyema mechi zake za Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Jeunesse Sportive de la Saoura, ijulikanayo kama JS Saoura au JSS jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Nyota wa mchezo wa leo alikuwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Arnold Okwi aliyefunga bao moja na kuseti mawili mawili mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa, Joshua Bondo aliyesaidiwa na washika vibendera Kitso Madondo Sibanda na Moemedi Monakwane wote wa Botswana, hadi mapumziko Simba SC walikuwa mbele kwa bao 1-0.

Bao hilo lilifungwa na mshambuliaji wake hodari, Okwi ‘Mtoa Roho’ dakika ya 45 na ushei kwa shuti kali baada ya ‘kuwapinduapindua’ mabeki wa JS Saoura kufuatia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chama.
Okwi aliyekuwa katika kiwango cha juu leo, alifunga bao hilo akitoka kukosa bao la wazi baada ya kugongesha nguzo ya juu akiwa tay... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More