SIMBA SC YAENDELEZA FURAHA KWA MASHABIKI WAKE, YAWAPIGA RUVU SHOOTING 2-0 TAIFA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMBA SC YAENDELEZA FURAHA KWA MASHABIKI WAKE, YAWAPIGA RUVU SHOOTING 2-0 TAIFA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SIMBA SC imeendeleza furaha kwa mashabiki wake baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku wa leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Ushindi huo unaifanya Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji, Patrick Aussems ifikishe pointi 54 baada ya kucheza mechi 21, sasa ikizidiwa pointi tano na Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwa pointi zake 59 za mechi 28, nyuma ya Yanga SC yenye pointi 67 za mechi 28.  
Baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Flerentina Zabron, Simba SC ilifunguka kipindi cha pili na kupata mabao yake yote mawili.

Kabla ya mchezo wake, Maddie Kagere alikabidhiwa tuzo yake ya kuwa Mchezaji Bora wa Ligi Kuu mwezi Februari

Alianza beki wa kati, Paul Bukaba Bundala kufunga la kwanza dakika ya 52 akimalizia shuti la kiungo Said Hamisi Ndemla baada ya mpira uliookolewa kufuatia krosi ya kiungo Mnyarwanda, Haruna Niyonzima aliyeanazishwa kona ... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More