SIMBA SC YAFUTA MAZOEZI KUMUOMBEA DUA MO DEWJI APATIKANE SALAMA BAADA YA KUTEKWA LEO ASUBUHI - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMBA SC YAFUTA MAZOEZI KUMUOMBEA DUA MO DEWJI APATIKANE SALAMA BAADA YA KUTEKWA LEO ASUBUHI

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
UONGOZI wa klabu ya Simba SC leo umefuta mazoezi kutokana na simanzi baada ya mfadhili wa klabu hiyo, mfanyabiashara Mohammed ‘Mo’ Dewji kutekwa mapema leo asubuhi na watu wasiojulikana.
Dewji alitekwa mapema leo asubuhi akiwa anaingia katika gym ya Collessium eneo la Masaki mjini Dar es Salaam kufanya mazoezi na tangu hapo Jeshi la Polisi linaendesha msako mkalio wa kumtafuta mfanyabiashara huyo.
Msemaji wa klabu ya Simba SC, Hajji Sunday Manara amesema kwamba kwa mashauriano na Benchi la Ufundi chini ya kocha Mkuu, Mbelgiji Patrick J. Aussems klabu imefuta mazoezi kutokana na simanzi iliyopo.
“Benchi la Ufundi chini ya Kocha Mkuu, Patrick Aussems limeamua kuahirisha mazoezi ya timu leo ili kutoa fursa kwa Wachezaji na Benchi la Ufundi kushiriki ipasavyo kwenye Dua na Sala kwa ajili ya kiongozi wetu,” amesema Manara.
Mohammed Dewji ametekwa leo asubuhi akiwa anaingia katika gym ya hoteli yab Collessium, Oysterbay mjini Dar es Salaam kufanya mazoezi... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More