SIMBA SC YAIGONGA AL AHLY 1-0 NA KUFUFUA MATUMAINI YA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMBA SC YAIGONGA AL AHLY 1-0 NA KUFUFUA MATUMAINI YA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SIMBA SC imefufua matumaini ya kwenda Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Al Ahly kwenye mchezo wa Kundi D jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Pongezi kwa mfungaji wa bao pekee katika mchezo huo, mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda mwenye asili ya Uganda, Meddie Kagere aliye katika msimu wake wa kwanza tu Simba SC tangu awasili kutoka Gor Mahia y Kenya.
Kagere alifunga bao hilo dakika ya 65 kwa shuti la mguu kulia akimalizia pasi ya kichwa ya Nahodha na mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, John Raphael Bocco kufuatia krosi ya beki Zana Coulibaly kutoka Burkina Faso.

Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi sita baada ya kucheza mechi nne ikipanda kwa nafasi moja hadi ya pili, nyuma ya Al Ahly wenye pointi saba na mbele ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yenye pointi nne na JS Saoura ya Algeria yenye pointi mbili.
Ikumbukwe JS Saoura wanaikaribisha AS Vita Saa 4:00 usiku wa leo Uwanja w... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More