SIMBA SC YAIGONGA KMC 2-1 KIRUMBA NA KUISHUSHA AZAM, SASA YAIPUMULIA YANGA SC - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMBA SC YAIGONGA KMC 2-1 KIRUMBA NA KUISHUSHA AZAM, SASA YAIPUMULIA YANGA SC

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
SIMBA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa 2-1 KMC, zote za Dar es Salaam katika mchezo uliofanyika Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 66 baada ya kucheza mechi 26 na kupanda hadi nafasi ya pili ikiizidi kwa wastani wa mabao tu, Azam FC inayoangukia nafasi ya tatu, huku Yanga SC ikiendelea kuongoza kwa pointi zake 74 za mechi 32.
Dalili mbaya kwa KMC zilianza kuonekana mapema tu, baada ya baada ya mchezaji wake, Aaron Lulambo kuumia dakika ya 20 na kushindwa kuendelea na mchezo, nafasi yake ikichukuliwa na Kelvin Kijiri.

Na dakika ya 22 mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Arnold Okwi akaifungia Simba SC bao zuri akimalizia mpira wa adhabu wa kiungo Mghana, James Kotei kumtungua ‘Burundi One’, Jonathan Nahimana.
Nahodha na mshambuliaji John Raphael Bocco aliikosa bao la awazi dakika ya 42, baada ya pasi ya kupewa pasi nzuri na mshambuliaji wa kimataifa... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More