SIMBA SC YAIPIGA NDANDA FC NA KUWEKA MKONO MMOJA KWENYE KOMBE LA LIGI KUU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMBA SC YAIPIGA NDANDA FC NA KUWEKA MKONO MMOJA KWENYE KOMBE LA LIGI KUU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
TIMU ya Simba SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa mabao 2-0 Ndanda FC ya Mtwara katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Ushindi wa leo unawafanya Wekundu hao wa Msimbazi wafikishe pointi 88 katika mchezo wao wa 35 wa msimu na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi tano zaidi ya watani wao wa jadi, Yanga ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.
Sasa Simba SC inatakiwa kushinda mchezo wake wa Jumanne dhidi ya Singida United Uwanja wa Namfua ili kutawazwa rasmi kuwa mabingwa tena wa Ligi Kuu.
 

Ushindi wa leo wa Simba SC inayofundishwa na kocha Mbelgiji, Patrick Aussems umetokana na mabao ya mshambuliaji wa kimataifa wa Rwanda, Meddie Kagere mwenye asili ya Rwanda ndani ya robo saa ya kwanza ya mchezo.
Kagere aliye katika msimu wake wa kwanza Simba SC tangu asajiliwe kutoka Gor Mahia ya Kenya, alifunga bao la kwanza dakika ya sita kwa shuti akimalizia pasi ya mshambuliaji mwenzake, Nahodha, John... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More