SIMBA SC YAONYESHA NI TISHIO, YATOA SARE NA BIG BULLETS LICHA YA KUWAKOSA NYOTA WAKE KIBAO WA KIKOSI CHA KWANZA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMBA SC YAONYESHA NI TISHIO, YATOA SARE NA BIG BULLETS LICHA YA KUWAKOSA NYOTA WAKE KIBAO WA KIKOSI CHA KWANZA

Na Nasra Omary, DAR ES SALAAM
SIMBA SC imedhihirisha siyo tu ina kikosi kipana, lakini pia imara baada ya kutoa sare ya 0-0 na Nyasa Big Bullets ya Malawi katika mchezi wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Pamoja na kuwakosa karibu wachezaji wake wote wa kikosi cha kwanza ambao wamechukuliwa na timu zao za taifa kwa ajili ya mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) ya wakubwa na ya vijana chini ya umri wa miaka 23, Simba ilicheza vyema na kukaribia kushinda.   
Simba SC, mabingwa wa Tanzania Bara leo walitengeneza nafasi zaidi ya tatu nzuri, lakini bahati mbaya umaliziaji ukawanyima japo bao moja katika mchezo huo mzuri. 
Kiungo Mnyarwanda wa Simba SC, Haruna Niyonzima akiondoka na mpira mbele ya mchezaji wa Big Bullets leo  
Kiungo Hassan Dilunga akituliza mpira kwa ustadi mkubwa leo Uwanja wa Taifa 
Mshambuliaji Mohammed Rashid akimpita beki wa Big Bullets, anayejaribu kuutelezea mpira

Kikosi cha Big Bullets kilichotoa sare ya bila kufungan... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More