SIMBA SC YAPATA MDHAMINI MPYA AMBAYE ATAWAJENGEA UWANJA MZURI BUNJU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMBA SC YAPATA MDHAMINI MPYA AMBAYE ATAWAJENGEA UWANJA MZURI BUNJU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAMKLABU ya Simba SC ya Dar es Salaam imeingia mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja na Kampuni ya A1 Products kupitia kinywaji cha Mo Energy Drink wenye thamani ya Sh. Milioni 250.
Hiyo ni moja ya makampuni yanayomilikiwa na mmiliki mtarajiwa wa klabu hiyo, Mohammed ‘Mo’ Dewji kupitia kampuni yake mama, Mohamed Enterprises Limited (MeTL)
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Kaimu Rais Simba SC, Salim Abdallah 'Try Again' amesema fedha zote za udhamini huo zitaenda katika mradi wa ujezi wa Uwanja mpya wa klabu huko Bunju.
Pamoja hayo, Simba SC leo imezindua jezi zake mpya za msimu ujao kwa ajili ya mashabiki wake ambazo zitakuwa zinauzwa kwa Sh. 25,000.
 
Simba SC imefanya yote hayo saa chache tu baada ya kurejea mjini Dar es Salaam leo Alfajiri kutoka nchini Uturuki ambako ilikwenda kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na msimu mpya.
Pamoja na mazoezi, ziara hiyo ilihusisha mechi mbili za kujipima nguvu kwanza sare ya 1-1 na MC Oujder ya M... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More