SIMBA SC YAPUNGUZWA KASI MTWARA, YAAMBULIA SARE 0-0 NA NDANDA NANGWANDA SIJAONA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMBA SC YAPUNGUZWA KASI MTWARA, YAAMBULIA SARE 0-0 NA NDANDA NANGWANDA SIJAONA

Na Mwandishi Wetu, MTWARA
MABINGWA watetezi, Simba SC leo wameshindwa kuendeleza ubabe wake kwa Ndanda FC baada ya kuambulia sare ya bila kufungana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Sare hiyo ya kwanza katika mechi ya kwanza ya ugenini baada ya kushinda mechi mbili mwanzoni nyumbani inamaanisha timu hiyo ya kocha Mbelgiji, Patrick J Aussems inafikisha pointi saba, wakati Ndanda FC inafikisha pointi nne katika mechi nne, baada ya kushinda moja awali na kufungwa mbili.
Aussems leo aliwaanzisha kwa pamoja washambuliai wake hatari, Nahodha  John Bocco, Mnyarwanda Meddie Kagere mwenye asili ya Uganda na Mganda Emmanuel Okwi lakini wote wakashindwa kufurukuta mbele ya safu ya ulinzi ya Ndanda iliyoongozwa na Malika Ndeule.

Mchezo wa kujihami ulionekana kuisaidia Ndanda FC ambayo baada ya kufungwa na Simba SC katika mechi zote za nyumbani na ugenini tangu ipande Ligi Kuu mwaka 2014 leo imemaliza salama chini ya kocha wake, Malale Ham... Continue reading ->

Source: Bin ZuberyRead More