SIMBA SC YATAJA VIINGILIO MAPEMA MECHI NA AS VITA JUMAMOSI UWANJA WA TAIFA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMBA SC YATAJA VIINGILIO MAPEMA MECHI NA AS VITA JUMAMOSI UWANJA WA TAIFA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KLABU ya Simba leo imetaja viingilio vya mchezo wake wa mwisho wa Kundi D Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Jumamosi wiki hii Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Sunday Manara amesema kwamba kiingilio cha chini katika mchezo huo kitakuwa ni Sh. 3,000 kwa majukwaa ya mzunguko.
Manara amesema kwamba viingilio vingine ni Sh. 20,000 kwa VIPA A, Sh. 10,000 kwa VIP B na Sh. 100,000 kwa tiketi maalum za Platinums.

Mchezo huo utakaoanza Saa 1:00 usiku, utachezeshwa na marefa wa Morocco, Noureddine El Jaafari atakayepuliza kipyenga na washika vibendera Hicham Ait Abbou na Yahya Nouali.
Simba SC inahitaji ushindi katika mchezo huo ili kutinga Robo Fainali, baada ya kupoteza mechi zake zote tatu za ugenini, 5-0 mara mbili dhidi ya Al Ahly nchini Misri na AS Vita mjini Kinshasa na 2-0 dhidi ya JS Saoura mjini Bechar. 
Kwa sasa JS Saoura ndiyo inayoongoza Kundi D k... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More