SIMBA SC YATIKISA KLABU BINGWA AFRIKA, YAINYUKA BILA HURUMA JS SAOURA YA ALGERIA 3-0 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMBA SC YATIKISA KLABU BINGWA AFRIKA, YAINYUKA BILA HURUMA JS SAOURA YA ALGERIA 3-0

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kimataifa Timu ya Simba imefanikiwa kuondoka na ushindi wa kwanza katika Kundi D baada ya kuifunga JS Saoura goli 3-0.
Simba wakiwa wako katika uwanja wa nyumbani wa Taifa walianza kwa kasi kulisakama lango la JS Saoura na ilichukua dakika 45 kwa Mshambuliaji Emanuel Okwi kuandika bao la kuongoza kwa shuti kali baada ya ‘kuwapinduapindua’ mabeki wa JS Saoura kufuatia pasi ya kiungo Mzambia, Clatous Chama.
Okwi aliyekuwa katika kiwango cha juu leo, alifunga bao hilo akitoka kukosa bao la wazi baada ya kugongesha nguzo ya juu akiwa tayari amemtoka beki anatazamana na kipa.    
Simba Walifanya mabadiliko dakika ya 34 wakimtoa Nahodha wake, John Raphael Bocco ‘Adebayor’ baada ya kuumia nafasi yake kuchukuliwa na mshambuliaji mwenzake, Meddie Ksgere kutoka Rwanda. 
Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kurudi na nguvu mpya na kufanikiwa kupata mabao mawili zaidi yote yakifungwa na Kagere Goli la pili akifunga dakika ya 51 akimalizia pasi ya O... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More