Simba yaibuka kidedea, yaitandika Al Ahly ya Misri - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Simba yaibuka kidedea, yaitandika Al Ahly ya Misri

 Na Zainab Nyamka, Globu ya JamiiWawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika Simba wamefanikiwa kushinda katika mchezo wao Kundi D dhidi ya Al ahly ya Misri. Mchezo huo ulioanza kwa kasi katika dakika 10 za Kipindi Cha kwanza timu hizo ziliweza kusomana na kushambulia kwa kupokezana.
Katika kipindi cha kwanza Simba walishindwa kutumia nafasi walizozipata ingawa walifanikiwa kupata kona kwa wingi. Dakika 45 za Kipindi cha kwanza kilimalizika timu zote zikienda mapumziko wakiwa wako 0-0.
Kipindi cha pili kilianza Al Ahly wakisakama lango la Simba, lakini umakini wa safu ya ulinzi ya Simba ikaa makini kuondoa mipira kwenye lango lao. Dakika ya 65, mchezaji wa Kimataifa kutoka Rwanda Meddie Kagere anaipatia Simba goli la kwanza akipokea pasi ya Zana Coulibaly baada ya kuwahadaa ngome ya ulinzi ya Al ahly.
Mpira uliendelea kwa kasi Simba wakilinda goli lao na kutafuta goli lingine zaidi huku Al ahly wakisaka la kusawazisha. Mpaka mpira unamalizika katika Uwanja wa Taifa Sim... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More