SIMBA YAUNGURUMA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO, YAIFUNGISHA VIRAGO AS VITA MATAIFA YA AFRIKA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMBA YAUNGURUMA UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR LEO, YAIFUNGISHA VIRAGO AS VITA MATAIFA YA AFRIKA

 Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Klabu ya Simba inafanikiwa kuingia katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya kuifunga timu ya As Vita goli 2-1  na kushika nafasi ya pili kwenye Kundi D.
Mechi hiyo imechezwa leo katika dimba la Uwanja wa Taifa na msumari wa ushindi uliwekwa na Clotous Chota Chama na kuivusha Simba kwenye hatua ya Makundi.
Ilikua dakika ya 12, As Vita wanaandika goli la kwanza kupitia kwa mchezaji wake Fabrice Ngoma na kuipa timu yake uongozi.
Katika dakika ya 32, Mohamed Hussein anaipatia Simba goli la kusawazisha na kwenda mapumziko wakiwa 1-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi Simba wakisaka goli la ushindi  na As Vita nao wakitafuta namna ya kupenya katika ngome ya ulinzi ya Simba.
Simba wanalisakama lango la As vita na wakipoteza nafasi nyingi za wazi mabadiliko ya kumtoa Emanuel Okwi na kuingia Haruna Niyonzima yaliweza kuzaa matunda na kurejesha uhai katika kikosi hicho.
Katika dakika ya 86, Simba wanafanya shambulizi langoni mwa As Vita... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More