Simba yaweka rekodi kubwa mauzo ya jezi, ndani ya miaka mitatu yaingiza mamilioni ya fedha - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Simba yaweka rekodi kubwa mauzo ya jezi, ndani ya miaka mitatu yaingiza mamilioni ya fedha

Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba SC kupitia kwa msemaji wake, Haji Manara amesema kuwa ndani ya miaka mitatu iliyopita klabu hiyo imefanikiwa kuingiza zaidi ya shilingi milioni 200 kutokana na mauzo ya jezi zake.Manara ameeleza kuwa Simba imefanikiwa kuweka rekodi hiyo ambayo ni kubwa kwa klabu za hapa nchini Tanzania.


Mkuu huyo wa kitengo cha habari ndani ya Wekundu wa msimbazi Simba ameongeza kuwa malengo ya mwaka huu ni kufikia milioni 300 kutoka kiasi cha awali ambacho ni 200.


Hapo jana siku ya Jumatatu ya tarehe 06/08/2018 klabu ya Simba ilizindua jezi zake mpya za msimu ujao wa 2018/19 huku bei elekezi kwa mawakala ni shilingi elfu 25,000.


The post Simba yaweka rekodi kubwa mauzo ya jezi, ndani ya miaka mitatu yaingiza mamilioni ya fedha appeared first on Bongo5.com.

... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More