Simbu apenya Olympic 2020 - Shaffih Dauda | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Simbu apenya Olympic 2020

Wanariadha wa Tanzania Alphonce Simbu na Augustino Sulle wamefanikiwa kufuzu kwa michezo ya Olympic itakayofanyika jijini Tokyo, Japan mwakani.

.

.

Wanariadha hao wamefanikiwa kufuzu baada ya kukimbia kwa muda mzuri kwenye mbio za Lake Biwa Marathon zilizofanyika Osaka Japan ambazo zinatambulika na kupitishwa na shirikisho la riadha la dunia.

.

.

Katika mbio hizo ambazo zilikuwa na ushindani kutoka wanariadha mbalimbali duniani, Simbu ambaue ni mshindi wa medali ya shaba ya dunia alimaliza katika nafasi ya 6 akiandika rekodi yake mpya ya akitumia saa 02:08:27. Rekodi ya awali ya Simbu kabla ya mashindano hayo ilikuwa saa 02:09:10 aliyoiweka London Marathon.

.

.

Kwa upande wa Sulle ambaye anashikilia rekodi ya taifa Marathoni ya saa 2:07:04 aliyoiweka Toronto, Canada mwaka jana, amemaliza nafasi ya 17 akitumia saa 02:12:42.

.

.

Muda wa kufuzu Olympic ambao unaanza kutambuliwa kuanzia January mwaka huu ni saa 02:14 kwa wanaume.... Continue reading ->


Source: Shaffih DaudaRead More