SIMIYU YAANDAA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAWEKEZAJI, YAAHIDI KUTOA ARDHI YA UWEKEZAJI BURE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMIYU YAANDAA MAZINGIRA WEZESHI KWA WAWEKEZAJI, YAAHIDI KUTOA ARDHI YA UWEKEZAJI BURE

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga akifungua Kongamano la Uwekezaji la Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali Waadiventista Wasabato (ATAPE), kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka, lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.

Na Stella Kalinga, Simiyu

Serikali mkoani Simiyu imesema imeandaa mazingira wezeshi kwa wawekezaji katika Fursa  mbalimbali za uwekezaji  ikiwemo viwanda, kilimo na teknolojia, ambapo imejipanga kutoa ardhi bure kwa wawekezaji walio tayari kuwekeza mkoani humo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga  ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo , Mhe. Anthony Mtaka katika Ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji la Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE), lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.

Kiswaga amesema mkoa huo ni mkoa wenye ajenda ya maendeleo, hivyo umejipanga katika kuwawekea mazingira mazuri wawekezaji katika fursa mbalimbali za uwekezaji mkoani humo, ikiwa ni pamoja na  sekta ya viwanda, kilimo, tekonolojia mbalimbali, uchimbaji wa visima na fursa nyingine, ili kufikia lengo la  kuufanya mkoa huo kuwa  katika nafasi nzuri kiuchumi.Mwenyekiti wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali Waadiventista Wasabato (ATAPE) Taifa, Bw. Fredy Manento, akitoa taarifa ya Chama hicho wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Uwekezaji la Chama hicho lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.

“Mkoa wa Simiyu una fursa nyingi mkifika hapa chagueni tu sehemu mje kuwekeza, mtu atakayekuja kujenga kiwanda kikubwa, kizuri ardhi tutampa bure, sisi tutamuuliza tu kwamba tuandike jina gani kwenye hati na tutamkabidhi hati yake, kwa hiyo ATAPE pelekeni salamu kwa wawekezaji wenzenu kuwa ardhi ya uwekezeaji Simiyu ni bure, ninyi mtafute mtaji tu” alisema Kiswaga.

Ameongeza kuwa wawekezaji wote watakaowekeza mkoani Simiyu watapata soko la uhakika la bidhaa zao, huku akibainisha kuwa mkoa wa Simiyu na mikoa inayouzunguka ina wakazi wasiopungua milioni 10 ambao watakuwa wanunuzi wakubwa wa bidhaa zao watakazozalisha.

Aidha, Kiswaga ametoa wito kwa wawekezaji wote wakiwemo ambao ni wanachama wa  Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali  Waadiventista Wasabato (ATAPE), kuwekeza katika ujenzi wa hoteli na hosteli katika Eneo la Nyakabindi mahali ulipo Uwanja wa Nanenane Halmashauri ya Mji wa Bariadi ili kukabiliana na changamoto ya malazi.
Baadhi ya Wanachama wa Chama cha Wanataaluma na Wajasiriamali Waadiventista Wasabato (ATAPE), wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (hayupo pichan) wakati akifungua Kongamano la Uwekezaji la Chama hicho lililofanyika Mjini Bariadi Septemba 13, 2018.

BOFYA HAPA KWA HABARI NA PICHA ZAIDI


Source: Issa MichuziRead More