SIMIYU YAZINDUA MFUMO WA MSHITIRI MMOJA KATIKA DAWA NA VIFAA TIBA , JAZIA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SIMIYU YAZINDUA MFUMO WA MSHITIRI MMOJA KATIKA DAWA NA VIFAA TIBA , JAZIA

Na Stella Kalinga, SimiyuKatibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  amezindua rasmi mfumo wa ununuzi wa dawa na vifaa tiba kupitia kwa mshitiri mmoja wa mkoa ujulikanao kama JAZIA, uliobuniwa kuboresha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, vifaa vya maabara na uchunguzi katika vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali ngazi ya Mkoa na Halmashauri.
Akizindua mfumo huo Novemba 05, 2018  Sagini amesema mfumo wa JAZIA si mbadala wa Bohari ya Dawa (MSD) bali unalenga kuziba upungufu wa dawa, vifaa tiba, vifaa vya maabara na uchunguzi katika Bohari ya Dawa (MSD).
“JAZIA ni mfumo uliobuniwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na wataalam washauri ili kuweza kuboresha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, vifaa vya maabara na uchunguzi katika vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali ngazi ya Mkoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, JAZIA si mbadala wa MSD bali ni msaidizi wa MSD inapokuwa haina bidhaa husika.” alisema.
Aidha, Sagini alibainisha kuwa mfumo huu utasaidia kupunguza g... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More