SINGIDA UNITED KUTUMIA UWANJA WA AZAM COMPLEX DHIDI YA COASTAL UNION - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SINGIDA UNITED KUTUMIA UWANJA WA AZAM COMPLEX DHIDI YA COASTAL UNION


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mchezo wa Kombe la Shirikisho Azam Sports Federation Cup (ASFC) kati ya Singida United na Coastal Union sasa kufanyika Jijini Dar es Salaam. Singida United wameuomba uongozi wa TFF kuuruhusu mchezo huo kuchezwa Jijini Dar badala ya Singida kutokana na ugumu wa ratiba ya ligi na FA.

Akitoa taarifa hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Singida United United Festo Sanga amesema kuwa Kutokana na Ugumu wa ratiba yetu ya Ligi na kombe la FA, Mchezo wao dhidi ya Costal Union wa kombe la FA sasa utachezwa Dar es Salaaam tar 23/02/2019 badala ya Namfua Singida  ulivyopangwa awali.

Amesema kuwa,  leo Jumatano wanacheza na Ndanda Fc huko Mtwara, hivyo kesho  timu inatakiwa iondoke Mtwara kurejea Singida ambapo kwa umbali wa Mtwara hadi Singida ni safari ya Siku mbili, hivyo timu ingefika Singida tarehe Februari 22.

Sanga ameeleza kuwa mechi yao dhidi ya Coastal itachezwa Feb  23 wakiwa nyumbani Namfua na wameona kuwa  Jambo hilo tumeona sio salama kwa Afya ya wachezaji na m... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More