SINGIDA UNITED YAMALIZA NAFASI YA TATU SPORTPESA SUPER CUP - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SINGIDA UNITED YAMALIZA NAFASI YA TATU SPORTPESA SUPER CUP

Na Mwandishi Wetu, NAKURU
TIMU ya Singida United imemaliza katika nafasi ya tatu kwenye michuano ya SportPesa Super Cup baada ya ushindi wa penalty 4-1 baada ya sare ya 1-1 dhidi ya wenyeji, Kakamega Homeboyz Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, Kenya.
Kwa mara nyingine, kipa Peter Manyika Junior ameibuka shujaa wa Singida United baada ya kuokoa penalti moja ya Kakamega, huku nyingine mbili zikiota mbawa. 
Na waliofunga penalti za Singida United ni Miraji Adam, Shafiq Batambuze, Danny Lyanga na winga Deus Kaseke aliyechaguliwa Mchezaji Bora wa Mechi, huku klabu yake ikizawadiwa kitita cha dola za Kimarekani 7, 500 na Kakamega wakipewa dola 5,000. 

Kwa mara nyingine, kipa Peter Manyika Junior ameibuka shujaa wa Singida United

Katika dakika 90 za mchezo huo, Wicklif Opondo alifunga bao la Kakamega na Danny Lyanga akawafungia Singida United.
Bingwa wa SportPesa Super Cup atapata dola za Kimarekani 30,000 pamoja na nafasi ya kwenda kucheza na klabu ya Everton Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More