Sista Fey Atangaza Kuwa Mkristo Kwa Ajili Ya Ndoa na Kibenten - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Sista Fey Atangaza Kuwa Mkristo Kwa Ajili Ya Ndoa na Kibenten

Msanii wa Bongo fleva Faidha Omary maarufu kama Sista Fey ametangaza kuwa Yupo Tayari kubadilisha dini yake kutoka kuwa Muislamu mpaka Ukristo kwa ajili ya ndoa.


Sista Fey ambaye yupo Kwenye mahusiano na msanii Elias John maarufu kama Hollystar wamekuwa wakitengeneza headlines kwa vituko vyao Kwenye mitandao ya kijamii.


Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Fey amesema kwa sasa wako kwenye mipango ya kuingia kwenye ndoa harakaharaka kwa kuwa ni mjamzito hivyo yupo radhi kubadili dini kwa sababu amependa kweli.Tuko kwenye mipango ya ndoa na ndani ya miezi miwili hii tutafunga ndoa, niko tayari kubadili dini, tunasubiri tu uamuzi kutoka kwa babamkwe kwamba tutafunga ndoa ya bomani au kanisani.


Sioni shida kubadili dini au kuolewa na kijana huyo, kisa namzidi umri kwa sababu hakuna asichokijua kwenye dunia hii, nampenda na siwezi kumuacha ndiyo maana niko tayari kubadili dini nimfuate kwenye ukristo kama mzazi wake ataamua hivyo”. 


The post Sista Fey Atangaza Kuwa Mkri... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More