Sister fey Aongea na Watanzania Kuhusu Kipaji Chake. - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Sister fey Aongea na Watanzania Kuhusu Kipaji Chake.

Mwanamama asiyeishiwa matukio katika mitandao ya kijamii, Faidha Omary maarufu kama Sister Fey amefunguka na kuiomba jamii ya kitanzania imuunge mkono katika kazi zake za sanaa azifanyajo huku akiwataka wasimuhukumu kwa mambo anayoyafanya mitandaoni bila ya kujua undani wake.


Sister Fey amebainisha hayo wakati alipokuwa anapiga stori na www.eatv.tv, baada ya muziki wake kushindwa kufika mbali kutokana na watu wengi kupenda kufuatilia mahusiano yake zaidi, ambayo amekuwa akiyaweka hadharani kupitia mitandaoo ya kijamii.


“Watu wengi wananichukulia mimi kama chizi kutokana na mambo ninayoyafanya lakini hawapaswi kunihukumu kwa kunitazama upande mmoja. Mimi ni mwanamuziki mzuri tu, na pengine katika wasichana watatu wanaofanya vizuri bongo basi mimi naweza nikawa namba mbili. Sijapata tu mtu wa kunionyesha katika jamii kuhusiana na kipaji changu nilichokuwa nacho”, amesema Sister Fey.


Mbali na hilo, Sister Fey amedai kwamba hiki anachokipitia kwa sasa ipo siku atajitokeza mbele ya wata... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More