Sitoacha kufanya siasa hadi wapinzani watakapo nielewa - Maalim Seif - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Sitoacha kufanya siasa hadi wapinzani watakapo nielewa - Maalim SeifKatibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema hatoacha kufanyakazi ya siasa hadi pale wapinzani wake watakapo muelewa kuwa yeye ni fundi wa siasa.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa Mkutano Maalum wa Jumuiya ya wanawake CUF (JUKECUF) uliofanyika katika ukumbi Mjid kiembe samaki Mjini Unguja,

Mkutano huo ulikuwa na lengo kula kiapo cha utii kutoka kwa kina mama dhidi ya maamuzi ambayo yatatolewa na viongozi wao mara baada ya hukumu ya kesi zilizoko Mahakamani.

Maalim Seif alieleza kuwa kuna Viongozi wakubwa ndani ya CCM wanafikiria kuwa yeye ameisha kisiasa na hana nafasi tena katika ulimwengu wa siasa, jambo ambalo alieleza kuwa yeye yuko makini na hakuna kiongozi yoyote wa Chama cha Mapinduzi ambaye anaweze kueleza chochote mbele yake,

"Na wafanye tu mambo yao lakini mwaka huu watamjua ni nani Seif kwa kitu ambacho nitawafanyia," alieleza Maalim Seif.

“Wamenichezea kwa muda mrefu lakini nasema sasa basi, wasubiri waone kitu ambacho nitawafanya mwaka, mchezomchezo basi... Continue reading ->
Source: Mwanaharakati MzalendoRead More