Snura ahofia ‘mzimu wa chura’ katika muziki wake (+video) - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Snura ahofia ‘mzimu wa chura’ katika muziki wake (+video)

Msanii wa muziki Bongo, Snura Mushi amesema kwa sasa kila anapoandika wimbo au kutoka kutoa ni lazima awasiliana na Baraza la Sanaa Taifa (Basata).


Muimbaji huyo anayetamba na ngoma ‘Vumbi la Mguu’ amesema analazimika kufanya hivyo ili kuepuka hasara anayopata pindi nyimbo zake zinapofungiwa na Basata.


“Kiukweli muda mwingi hadi nikirekodi huwa napiga simu, nafanya hivyo kwa sababu sitaki tena kuona natengeneza kazi ikienda kule wanai-block, napata hasara kwa kweli halafu inakuwa si lengo,” Snura ameiambia Bongo5.


Utakumbuka mwaka 2016 wimbo wa Snura ‘Chura’ uliingia kwenye headline za ujito wa juu kutokana na maudhi yake kuonekana kwenda kinyume na maadili kitu kilichopekea wimbo huo na video yake kufungiwa na Basata.


Loading...Jiunge na Bongo5.com sasa
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More