Soko kubwa la bidhaa za kilimo EAC chachu ya maendeleo - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Soko kubwa la bidhaa za kilimo EAC chachu ya maendeleo

WATANZANIA wametakiwa kutumia ukubwa wa soko la Afrika Mashariki kujiinua kiuchumi kupitia bidhaa zilizoboreshwa za kilimo.Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji),Dk. Doroth Mwaluko kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa saba wa kitaifa wa utafiti wa uunganishaji wa mifumo ya kuinua uchakataji wa bidhaa za kilimo (7th NRG) uliofanyika ukumbi wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii-ESRF.Katika hotuba yake hiyo kwenye Mkutano  huo uliokuwa unazungumzia mnyororo wa thamani katika kilimo kwa Afrika Mashariki,iliyosomwa na Ezamo Maponde kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maendeleo ya Sekta Binafsi alisema ukubwa wa soko unaleta maana zaidi kama mifumo itaoanisha kuwezesha ukuaji wa soko na huduma zake.Alisema katika mkutano huo kwamba Afrika Mashariki ina jumla ya wananchi milioni 172 huku asilimia 22 ya wananchi wake wakiishi katika miji.Aidha alisema takwimu zinaonesha kwamba nchi hizo zina pato la taifa za dola za Marekani bilioni 172 kuf... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More