SPORTPESA YAZINDUA 'DILI' LA WATU KUJISHINDIA BAJAJI MPYA KILA SIKU - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SPORTPESA YAZINDUA 'DILI' LA WATU KUJISHINDIA BAJAJI MPYA KILA SIKU

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KAMPUNI ya kubashiri michezo nchini ya SportPesa leo imezindua rasmi promosheni ya kuinua maisha kiuchumi SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA itakayodumu kwa siku 100 ambapo mshindi ataweza kujishindia BAJAJ RE mpya, pesa taslimu au vyote kwa pamoja. Promosheni ya SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA inaanza leo Alhamisi 20 Septemba 2018. 
Akizungumza kwenye uzinduzi wa promosheni hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Tarimba Abbas amesema kuwa hii ni mara ya pili kwa kampuni hiyo kuendesha promosheni kama kwa wateja wake. ‘Mwaka jana tuliendesha promosheni kama hii – Shinda na SportPesa ambapo tulitoa bajaj 100 kwa washindi wetu. Washindi walitoka kwenye mikoa yote 23 ya Tanzania na waliweza kubadilisha maisha kwa kujiongezea kipato cha kila siku kupitia bajaj ambazo wengi wao waliweza kuzitumia kwa ajili ya biashara. Nia yetu sisi SportPesa ni kuendelea kuinua na kubadilisha maisha ya Watanzania kupitia michezo," alisema Tarimba.... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More