Stamina Atoa Siri Ya Mke Wake Kumzalia Mtoto Wa Kiume - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Stamina Atoa Siri Ya Mke Wake Kumzalia Mtoto Wa Kiume

Msanii wa muziki wa Hip hop nchini Boniventure Kabogo maarufu kama Stamina amefunguka na kuweka wazi kuwa mke wake aliyefunga naye ndoa miezi michache iliyopita anatarajia kumzalia mtoto wa kiume.Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Stamina alisema anatarajia kupata mtoto wakati wowote kuanzia sasa na kwamba siku hizi teknolojia imerahisisha mambo ambapo wanandoa mnaweza mkapanga muda gani mpate mtoto na awe wa jinsia gani, huku akifunguka zaidi kuwa endapo atapata mtoto wa kiume atamuita Lionel na kama akiwa wa kike atamuita Antonella.Kila kitu kinaenda sawa na muda wowote mke wangu anaweza akanipa mtoto, sababu ya kuwapa majina hayo ni kwamba nampenda sana Lionel Messi wa Barcelona, hivyo mwanangu wa kiume nitamuita Lionel kuonyesha ni kiasi gani namkubali yule mchezaji“. 


The post Stamina Atoa Siri Ya Mke Wake Kumzalia Mtoto Wa Kiume appeared first on Ghafla! Tanzania.... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More