Steve Nyerere Agoma Kumjibu Mama Kanumba. - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Steve Nyerere Agoma Kumjibu Mama Kanumba.

Msanii wa maigizo ya vichekesho nchini , stve nyerere amekiri kuwa kamwe hawezi kujibishana na mama wa msanii marehemu steven kanumba kwa sababu ana mheshimu sana kama mama yake.akiongea na EATV, steve amesema kuwa kamwe kwake itakuwa ni kukosa adabu kama atamjibu mama huyo.


Ameyaongea hayo ikiwa ni kukataa kujibu tuhuma na maneno aliyowahi kuyaongea mama huo kuhusu Steve nyerere hapo awali na huko akisema kuwa hamjui Steve tangu hata marehemu alipokuwepo hakukuwa na mahusiano mazuri baina yao.


Mama kanumba aliwahi kusema kuwa kwake itakuwa kitu cha ajabu kuona steve nyerere ana mpenda kwa sababu hakuwahi kumpenda hata marehemu, kauli ambayo ilizua sana utata katika mitandao ya kijamii kutoka kwa mama huyo.


Ni zaidi ya mara moja mama huyo na steve wamekuwa wakirushiana maneno katika mitandao ya kijamii  hasa kipndi mahakama ilipofanya mabadiliko ya kesi ya mwanadada lulu ambapo mama huyo aliona kama wameonewa kwa kitu hicho na ndipo walikuwa wakirumbana sana na steve.


 


The post Stev... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More