SUDAN: JESHI NA WAANDAMANAJI WAKUBALIANA KUUNDA SERIKALI YA MPITO - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

SUDAN: JESHI NA WAANDAMANAJI WAKUBALIANA KUUNDA SERIKALI YA MPITO

Jeshi la Sudan

Viongozi wa kijeshi nchini Sudan na viongozi wa waandamanaji wamekubaliana kuunda serikali ya mpito, itakayo kuwa madarakani kwa muda wa miaka mitatu, na hatimaye madaraka kukabidhiwa kikamilifu kwa uongozi wa kiraia.
Makubaliano haya yamekuja, baada ya mazungumzo yaliyoanza mwishoni mwa wiki iliyopita kuonekana kuzaa matunda, kutokana na waandamanaji kuendelea kushinikiza kuwa wanataka jeshi liachie madaraka baada ya zaidi ya miaka 30.
Jeshi kupitia Jenerali Yasser al-Atta limesema kuwa makubaliano hayo yatatiwa saini na pande zote mbili ndani ya saa 24 zijazo ili kuanza kutekelezwa.
Aidha, amewahakikishia wananchi wa Sudan kuwa makubaliano hayo yatatekelezwa kikamilifu ili kufikia matamanio ya raia wa taifa hilo.
Miongoni mwa makubaliano yaliyoafikiwa ni pamoja na bunge kuwa na wabunge 300 huku asilimia 67 wakitoka kwenye vuguvugu la waandamanaji, linalofahamika kama Alliance for Freedom and Change.
Maelfu ya waandamanaji kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa wameendelea kupiga kambi nje ya makao... Continue reading ->Source: Mwanaharakati MzalendoRead More