Sudan mambo bado, mazungumzo ya kuunda baraza la kiraia yaahirishwa, pande mbili zashindwa kuafikiana - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Sudan mambo bado, mazungumzo ya kuunda baraza la kiraia yaahirishwa, pande mbili zashindwa kuafikiana

Mazungumzo ya kuunda baraza la kiraia nchini Sudan yameahirishwa kwa mara nyingine huku pande zinazozungumza zikishindwa kupata muafaka kuhusu muundo wa baraza hilo la mpito kabla ya uchaguzi.


Sudan Protest (picture-alliance/AA/M. Hjaj )


Baraza la mpito la kijeshi na wawakilishi wa makundi ya upinzani nchini Sudan wameshindwa tena kuafikiana kuhusu kuundwa kwa chombo kipya kitakachotawala taifa hilo, wakati mazungumzo baina yao yakikabiliwa na mkwamo kuhusu watawala wa chombo hicho, kati ya wanajeshi ama raia.


Baraza hilo le kijeshi na wawakilishi hao wa makundi ya upinzani walikutana tena kwenye kasri la rais kuanzia Jumatatu jioni kuhitimisha mapendekezo ya muundo wa chombo hicho, lakini hawakufanikiwa kufikia makubaliano.


Hakuna upande uliozungumzia kuhusu kurejea kwa mazungumzo hayo, lakini mmoja wa viongozi wa waandamanaji Siddiq Yousef aliwaambia waandishi wa habari kwamba mazungumzo yalisitishwa tena hadi kutakapopatikana suluhu kati yao na baraza na kijeshi.


Afrika | Protests im Sudan (picture-alliance/dpa/AA/M. Hjaj)Waandamanaji nchini Suda wanataka serikali ya mpito ya kirai... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More